Swali: Je, mtu aseme kuwa makafiri wana akili sana kutokana na maendeleo ya uvumbuzi waliyofikia na mengineyo kwa dalili ya maneno ya Allaah:

يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ

“Wanajua ya juujuu katika mambo ya uhai wa dunia, lakini kuhusu Aakhirah wameghafilika [nayo].” (30:07)

Jibu: Waambie kuwa ni wajinga. Haijalishi kitu hata kama ni wasomi katika mambo ya uvumbuzi na elimu ya kidunia, ni wajinga wasojua kitu kuhusiana na mambo ya Aakhirah. Ni wajinga. Elimu hii haitowafaa kitu mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020