Swali: Kuna kitabu kilichozungumzia majina na sifa za Allaah unachowapendelea wanafunzi? Ni yapi maoni yako juu ya kitabu “al-Qawaa´id al-Muthlaa fiy Ma´rifat-il-Asmaa´ Allaahi al-Husnaa” cha Shaykh Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)?

Jibu: Ni kitabu kizuri na mwandishi wacho ni mwanachuoni mtukufu. Bila ya shaka ni kitabu kizuri na chenye kunufaisha. Allaah amjaze kheri.

Majina na sifa za Allaah zimeenea katika Qur-aan. Ukisoma Qur-aan utaona majina na sifa za Allaah kwa kiasi kikubwa.

Vilevile kuna kitabu cha Imaam Ibn Khuzaymah kinachoitwa “Tawhiyd”. Humo ametaja majina na Sifa zilizothibiti. Ni kitabu kizuri.

Vilevile [al-´Aqiydah] al-Waasitwiyyah, al-Hamawiyyah na at-Tadmuriyyah, vyote vimegusia maudhui haya ya majina na sifa za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020