Hatusemi lolote kuhusu Pepo isipokuwa kwa dalili

Swali: Je, Peponi kuna maamrisho ya kushusha macho chini [kutowaangalia wanawake]? Je, ni sahihi ya kwamba al-Huur al-´Ayn hawawi wakubwa na wala hawabadiliki?

Jibu: Hatusemi kitu isipokuwa kilichothibiti kwa dalili. Peponi hakuna mambo ya kuwakodolea macho wanawake kama Alivyoamrisha Allaah:

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ

“Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao [wasitazame yaliyoharamishwa kwao].” (24:30)

Watu wa Peponi watakuwa wenye kukinaika. Hawatokuwa na haja ya kukodoa macho kwa kuwa Peponi mna neema ambazo hazitowapatia nafasi ya kusema watazama kadhaa na kadhaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-4-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020