Ni kweli kwamba kuna tofauti katika masuala haya, lakini ni kitu gani kinachowaua watu hawa? Watu hawa hawatafiti. Kwa sababu wanachotaka ni kuyaacha mambo kama yalivo na kusema:
”Kuna maoni tofauti katika masuala haya. Kila mmoja achukue kila anachokitaka.”
Hapana! Zipo Hadiyth juu ya masuala haya.
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba kupewa maji na akapewa. Baada ya hapo kukabaki maji ndani ya glasi. Ni upande gani wa kulia unatakiwa kuzingatiwa hivi sasa? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuliani mwake alikuweko Ibn ´Abbaas. Kushotoni mwake alikuweko Abu Bakr. Akamuuliza Ibn ´Abbaas kama anamruhusu ampe Abu Bakr, lakini Ibn ´Abbaas akakataa ampe mabaki yake mtu mwengine. Hivyo akampa yeye na akasema:
”Fuatisheni kuliani.”
Wewe, ambaye ni mhudumu, umeingia kupitia kule. Upande wako wa kulia ni kule, na si kule.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (548)
- Imechapishwa: 18/12/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)