Swali: Ni ipi tofauti kati ya waasi na Khawaarij?

Jibu: Khawaarij wanawakufurisha waislamu wakati waasi wanafanya uasi na kumuasi mtawala na hawawakufurishi waislamu. Kwa ajili hiyo wanadai kwamba huko ni kuamrisha mema na kukataza maovu. Huku ni kuvuka mipaka. Mema yanaamrishwa na maovu yanakatazwa kwa kuwepo uwezo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ambaye katika nyinyi ataona maovu ayaondoshe kwa mkono wake. Ikiwa hawezi, afanye hivo kwa ulimi wake. Ikiwa hawezi, afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”

Kuamrisha mema na kukataza maovu kunatokamana na uwezo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20%20-%204%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017