Swali: Ni ipi hukumu ya upasuaji wa plastiki? Ni nini hukumu ya kusomea upasuaji wa plastiki?
Jibu: Kuna aina mbili ya upasuaji wa plastiki:
1 – Kwa lengo la kuondoa kasoro inayotokana na ajali na mfano wake. Haina neno kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa idhini yule bwana ambaye ilikatwa pua yake aweke pua ya bandia ya dhahabu.
2 – Kuzidisha urembo. Ni haramu na haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kuondoa nywele za usoni na mwanamke mwenye kuomba kuondolewa nywele za usoni, mwanamke mwenye kurefusha nywele zake na mwanamke mwenye kuombwa kurefushiwa nywele zake, mwanamke mwenye kufanya chanjo na mwanamke mwenye kuomba kutiwa chanjo.”[1]
Kwa sababu huko ni kuongeza urembo ambao hauihusiani na kuondoa kasoro.
Kuhusiana na mwanafunzi anayesomea upasuaji wa plastiki kwenye silebasi yake ya masomo, hapana vibaya kuisomea lakini asiitumie katika zile hali ambazo ni haramu. Bali mtu anayesomea masomo hayo awashauri wale wanaotaka kufanya hivo kujiepusha kwa sababu ni haramu. Pengine nasaha zikitoka kwa daktari zikawa na uzito zaidi kwa watu.
[1] al-Bukhaariy (5943) na Muslim (2125).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/22)
- Imechapishwa: 03/06/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya upasuaji wa plastiki? Ni nini hukumu ya kusomea upasuaji wa plastiki?
Jibu: Kuna aina mbili ya upasuaji wa plastiki:
1 – Kwa lengo la kuondoa kasoro inayotokana na ajali na mfano wake. Haina neno kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimpa idhini yule bwana ambaye ilikatwa pua yake aweke pua ya bandia ya dhahabu.
2 – Kuzidisha urembo. Ni haramu na haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kuondoa nywele za usoni na mwanamke mwenye kuomba kuondolewa nywele za usoni, mwanamke mwenye kurefusha nywele zake na mwanamke mwenye kuombwa kurefushiwa nywele zake, mwanamke mwenye kufanya chanjo na mwanamke mwenye kuomba kutiwa chanjo.”[1]
Kwa sababu huko ni kuongeza urembo ambao hauihusiani na kuondoa kasoro.
Kuhusiana na mwanafunzi anayesomea upasuaji wa plastiki kwenye silebasi yake ya masomo, hapana vibaya kuisomea lakini asiitumie katika zile hali ambazo ni haramu. Bali mtu anayesomea masomo hayo awashauri wale wanaotaka kufanya hivo kujiepusha kwa sababu ni haramu. Pengine nasaha zikitoka kwa daktari zikawa na uzito zaidi kwa watu.
[1] al-Bukhaariy (5943) na Muslim (2125).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/22)
Imechapishwa: 03/06/2026
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-ya-upasuaji-wa-wa-vipodozi-na-plastiki/