Ni ipi hukumu ya swalah ya mwanamke bila ya mtandio?

Swali 257: Ni ipi hukumu ya swalah ya mwanamke bila ya mtandio?

Jibu: ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah ya mwenye hedhi isipokuwa akiwa na mtandio.”

Hadiyth imefahamisha kwamba swalah ya mwanamke haikubaliwi isipokuwa kwa mtandio unaofunika kichwa chake. Makusudio ya mwenye hedhi ni yule mwanamke ambaye ´ibaadah ni zenye kumuwajibikia ambaye kishabaleghe. Hakusudiwi yule ambaye yumo ndani ya siku zake. Kwa sababu hedhi inazuia swalah. Kumetajwa hedhi kwa kuzingatia kile kinachotokea mara nyingi. Vinginevyo endapo atabaleghe kwa kuota kwa mfano basi itamgusa hukumu iliyotajwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 98
  • Imechapishwa: 30/09/2019