Ni ipi hukumu ya mtu kuwaombea maiti na kujiombea mwenyewe kwenye kaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan tukufu makaburini? Ni ipi hukumu ya kuwaombea du´aa maiti na mtu kujiombea mwenyewe makaburini?

Jibu: Kusoma Qur-aan makaburini ni Bid´ah. Halikupokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake. Mambo yakishakuwa ni hivo tusizue kutoka kwenye nafsi zetu. Imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninakutahadharisheni na Bid´ah, kwani hakika kila Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.”[1]

Ni wajibu kwa waislamu wawaige Salaf katika Maswahabah na waliowafuata kwa wema mpaka wawe juu ya kheri na uongofu. Imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika maneno bora kabisa ni maneno ya Allaah na uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Ama kumuombea du´aa maiti kwenye kaburi lake haina neno. Asimame karibu na kaburi lake na amuombee kwa Allaah amsamehe, amrehemu, amwingize Peponi, ampanulie kaburi lake na mfano wa hayo.

Kuhusu mtu kujiombea du´aa mwenyewe kwenye kaburi, kitendo hichi ni Bid´ah ikiwa alikusudia kufanya hivo. Kwa kuwa amekhusisha ´ibaadah sehemu pasi na dalili ya hilo. Hakuna dalili katika Sunnah juu ya sehemu maalum kwa ajili ya du´aa. Pasi na kujali pahali hapo palipokhusishwa kitendo hicho kinakuwa ni Bid´ah.

[1] Muslim (867).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/227-228)
  • Imechapishwa: 02/09/2021