Ni ipi hukumu ya kumuombea maiti du´aa ya pamoja baada ya kuzika?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuomba du´aa ya pamoja ambapo mmoja anaomba du´aa na wengine wanaitikia “Aamiyn”?

Jibu: Hii sio Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala ya makhaliyfah wake waongofu (Radhiya Allaahu ´anhum). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaambia wamtakie msamaha na uthabiti yule maiti. Kila mmoja anatakiwa kufanya hivo kivyake na isiwe kwa pamoja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/228-229)
  • Imechapishwa: 02/09/2021