Ni ipi hukumu ya mawaidha wakati wa mchakato wa mazishi?

Swali: Unasemaje juu ya wale wenye kutoa mawaidha wakati wako wanamzika maiti? Kuna tatizo kudumu juu ya kitendo hicho?

Jibu: Naonelea kuwa kitendo hichi sio Sunnah. Kwa kuwa hakikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Kubwa lililopokelewa ni kuwa siku moja (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwenda kwenye jeneza la Answaariy mmoja akakaa yeye na wengine wakisubiri azikwe. Hapo ndipo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaeleza yanayompitikia mwanadamu pindi anapokufa na baada ya kuzikwa. Mara nyingine alisimama (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) karibu na kaburi wakati wa mazishi akasema:

“Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa ameshaandikiwa makazi yake Peponi na makazi yake Motoni.”[1]

Lakini hakusimama na kuanza kuwakhutubia kama wanavyofanya baadhi ya watu hii leo. Alikuwa amekaa na akazungumza nao kama katika kikao. Isitoshe hakufanya hivo kama ada. Kwa mfano hakuna neno wakati kunaposubiriwa watu wakazungumza mfano wa maongezi kama haya. Ni Sunnah. Ama kusimama mtu na akaanza kuwakhutubia watu sio katika Sunnah. Isitoshe mawaidha kama haya kabla ya mazishi yanazuia mchakato wa mazishi usiharakishwe.

[1] al-Bukhaariy (1362) na Muslim (2647).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/233-234)
  • Imechapishwa: 02/09/2021