Swali: Ni ipi hukumu ya kutaja mazuri ya maiti? Ni ipi hukumu ya kumuombea du´aa baada ya kuzikwa? Ni ipi hukumu ya kuwaomba wahudhuriaji wamuombee?

Jibu: Kutaja mazuri ya maiti hakuna neno midhali sio kwa njia ya kuomboleza. al-Haakim amepokea katika “al-Mustadrak” yake kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika mazishi ya Banuu Salamah na mimi nilikuwa karibu naye. Baadhi yao wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Alikuwa mwanaume mzuri. Alikuwa ni muislamu safi.” Wakamsifu vizuri ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Wewe unasemaje?” Mtu yule akasema: “Allaah ndiye anajua yale yaliyofichikana.”[1]

Kuhusu kumuombea maiti baada ya mazishi au kuomba du´aa, Abu Daawuud amepokea ya kwamba ´Uthmaan bin ´Affaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anapomaliza kumzika maiti husimama na kusema: “Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti. Hakika hivi sasa ataulizwa.”[2]

Mtu akifanya hivo na mfano wake haina neno.

[1] Tazama ”Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym” (1/348) ya Ibn Kathiyr.

[2] Abu Daawuud (3221).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/236)
  • Imechapishwa: 02/09/2021