Ni ipi hukumu ya kuyanyunyizia maji makaburi ili udongo uwe imara?

Swali: Ni ipi hukumu ya kunyunyuzia maji kwenye kaburi kwa kuwa kunafanya udongo kuwa imara?

Jibu: Hakuna neno kunyunyizia maji. Maji yanaufanya udongo kuwa imara na kutoenda huku na kule. Ama yale yanayoitakidiwa na wasiokuwa wasomi wanaoyanyunyizia maji makaburi ili kuwafanya wale maiti wapate baridi, ni jambo lisilokuwa na asli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/194)
  • Imechapishwa: 25/08/2021