Swali: Ni ipi hukumu ya kulinyanyua kaburi?

Jibu: Kulinyanyua kaburi ni kwenda kinyume na Sunnah. Ni wajibu kulisawazisha liwe sawa na makaburi mengine yaliyo pembezoni mwake au kuyashusha katika ule urefu wa kawaida. ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nisikutume katika yale aliyonituma Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Usiache picha isipokuwa umeiharibu na wala kaburi lililonyanyuliwa isipokuwa umelisawazisha.”[1]

[1] Muslim (969).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/185)
  • Imechapishwa: 25/08/2021