Ni ipi hukumu ya kuweka jiwe au mawe mawili karibu na kaburi la mwanamke?

Swali: Ni ipi hukumu kwa yule anayeweka pembezoni na kaburi la mwanaume mawe mawili na pembezoni na kaburi la mwanamke jiwe moja?

Jibu: Utofautishaji huu haukuwekwa katika Shari´ah. Wanachuoni wanasema kuwa haina neno kuweka jiwe moja au mawili pembezoni na kaburi kama alama ili litambulike na lisichimbwe kwa mara ya pili. Kuhusu kutofautisha kati ya kaburi la mwanaume na la mwanamke, ni jambo lisilokuwa na asli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/186)
  • Imechapishwa: 25/08/2021