Ni ipi hukumu ya kumsomea maiti Qur-aan na kuiweka juu ya tumbo lake?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma Qur-aan tukufu kwa maiti na kuweka msahafu juu ya tumbo lake? Kutoa pole kuna kikomo cha idadi ya masiku? Inasemekana kuwa ni siku tatu.

Jibu: Hakuna asli sahihi juu ya kumsomea Qur-aan maiti na kusoma karibu na kaburi la yule maiti. Sio jambo limewekwa katika Shari´ah. Bali ni Bid´ah.

Kadhalika kuweka msahafu juu ya tumbo lake ni jambo halina asli. Halikuwekwa katika Shari´ah. Walichosema baadhi ya wanachuoni ni kwamba kuwekwe kipande kidogo cha chuma au kitu kizito juu ya tumbo la maiti ili lisivimbe.

Kuhusu kutoa pole, hakuna kikomo cha masiku kadhaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/216)
  • Imechapishwa: 25/08/2021