Ni ipi hukumu ya kuandika kwenye majiwe ya makaburi au kuyapaka rangi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuandika kwenye majiwe ya makaburi au kuyapaka rangi?

Jibu: Kuyapaka rangi kunaingia katika sampuli ya kuyatia chokaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuyatia chokaa makaburi. Ni njia inayopelekea watu kuanza kushindana ni nani anayepaka rangi vizuri. Hatimaye makaburi yawe ni sehemu ya magambo. Kwa ajili hiyo ni wajibu kuliepuka. Kuhusu kuliandika, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuyaandika makaburi. Lakini baadhi ya wanachuoni wanasema ni sawa endapo lengo ni kutaka kutambua kaburi ni la nani na si matapo wala sifa. Katika hali hiyo makatazo itakuwa ni yale maandishi ya kumuadhimisha yule maiti kwa dalili kwamba hilo ni sambamba na makatazo ya kuyatia chokaa na kuyajengea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/189-190)
  • Imechapishwa: 25/08/2021