Ni ipi hukumu ya kuvua viatu pindi mtu anapoingia makaburini?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvua viatu wakati wa kuingia makaburini?

Jibu: Kutembea baina ya makaburi na viatu ni jambo linaloenda kinyume na Sunnah. Midhali hakuna haja lililo bora ni mtu kuvua viatu anapopita kati ya makaburi. Ikiwa makaburini kuna miba au ardhi ina joto kali au changarawe zinazoudhi haina neno kuvaa viatu pindi mtu anapotembea kati ya makaburi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/202)
  • Imechapishwa: 25/08/2021