Ni ipi hukumu ya kuweka alama fulani kwenye kaburi au kuandika jina la maiti juu yake?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka alama kwenye kaburi au kuandika jina la maiti kwa hoja ya kumtembelea?

Jibu: Ni sawa kuweka alama ya kama jiwe au mti.

Kuhusu kuandika juu yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuandika juu ya makaburi[1]. Lakini kukiandikwa jina tu pasi na matapo, sifa, Aayah za Qur-aan na mfano wa hayo, baadhi ya wanachuoni wanasema kuwa haina neno. Wanachuoni wengine wanasema kuwa hata kuandika jina kunaingia katika makatazo. Wanasema badala ya kuandika mtu anaweza kuchora alama fulani inayofahamisha kabila ya mtu. Wanasema hili linatosha. Hili ndio bora. Ikiwa alama inatosha basi hakuna haja ya kuandika.

[1] at-Tirmidhiy (1052) aliyesema ni nzuri na Swahiyh

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/190)
  • Imechapishwa: 25/08/2021