Ni ipi hukumu ya kumlaza maiti kwa mgongo na kuweka mikono yake juu ya tumbo?

Swali: Katika baadhi ya miji wanawazika maiti kwa kuwalaza kwa migongo yao na wanaiweka mikono yao juu ya tumbo zao. Ni ipi sahihi?

Jibu: Sahihi ni kuwa maiti anazikwa kwa kulazwa upande wake wa kulia hali ya kuuelekeza uso wake Qiblah. Ka´bah ndio Qiblah cha watu waliohai na maiti. Kama ambavyo mtu analala kwa upande wake wa kulia, kama alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), vivyo hivyo maiti anatakiwa kulazwa kwa upande wake wa kulia. Usingizi na kifo vina ushirikiano kwa vyote viwili kuwa vifo. Allaah (Ta´ala) amesema:

اللَّهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَى عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَى إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

“Allaah anazifisha nafsi wakati wa kufa kwake na zile zisizokufa katika usingizi wake. Huzizuia zile ambazo amezihukumia mauti na huzituma nyingine mpaka katika muda maalumu uliopangwa. Hakika katika hayo bila shaka kuna ishara kwa watu wanaozingatia.”[1]

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَى أَجَلٌ مُّسَمًّى ثُمَّ إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Yeye ndiye anayekufisheni usiku na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliopangwa. Kisha Kwake pekee ndio marejeo yenu, halafu atakujulisheni kuhusu yale yote mliyokuwa mkiyatenda.”[2]

Lililowekwa katika Shari´ah ni kumlaza maiti upande wake wa kulia hali ya kuuelekeza uso wake Qiblah. Pengine muulizaji aliona kitendo kinachotokamana na mtu mjinga. Vinginevyo sijui mwanachuoni yeyote anayesema kuwa maiti anatakiwa kulazwa kwa mgongo na kuiweka mikono yake juu ya tumbo lake.

[1] 39:42

[2] 6:60

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/182-183)
  • Imechapishwa: 25/08/2021