Ni ipi hukumu ya kuwazika Ahl-ul-Bid´ah kwenye makaburi ya Ahl-us-Sunnah?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwazika Ahl-ul-Bid´ah kwenye makaburi ya Ahlus-Sunnah?

Jibu: Ikiwa mzushi huyo Bid´ah zake ni zenye kumtoa katika Uislamu haijuzu kumzika pamoja na waislamu. Ni wajibu makaburi ya makafiri yawe ni yenye kutengana na makaburi ya waislamu. Ama ikiwa Bid´ah zake sio zenye kumtoa katika Uislamu haina neno kumzika pamoja na waislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/215)
  • Imechapishwa: 25/08/2021