Ni ipi hukumu ya dini kulijenga kaburi kwa matofali na simenti juu ya uso wa ardhi?

Swali: Ni ipi hukumu ya dini kulijenga kaburi kwa matofali na simenti juu ya uso wa ardhi?

Jibu: Kwanza mimi nachukia mtu kuuliza kwa njia kama “Ni ipi hukumu ya dini?”, “Ni ipi hukumu ya Uislamu?” na mfano wa hivo. Hakuna anayeabiria juu ya Uislamu kwa kuwa anaweza kukosea na kupatia. Tukisema kuwa anaabiria juu ya Uislamu, ina maana kuwa hawezi kukosea, kwa kuwa Uislamu hauna makosa. Kwa ajili hiyo bora ni kuuliza kwa njia kama “Unasemaje?”, “Unaonaje?” na mfano wa hivo.

Kuhusu swali, sionelei kuyajengea makaburi. Imethibiti ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuyajengea makaburi, kukaa juu yake na kuyatia chokaa[1]. Kwa hiyo kuyajengea makaburi ni haramu kwa kuwa ni njia inayopelekea yakaabudiwa na kushirikishwa pamoja na Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Muslim (970).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/212-213)
  • Imechapishwa: 25/08/2021