Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Matamshi ya imani hayakamiliki isipokuwa kwa matendo, wala matamshi na matendo isipokuwa pamoja na nia, wala matamshi, matendo na nia isipokuwa kwa kuafikiana na Sunnah.

MAELEZO

Imani inaweza kuwa imani kamilifu au pungufu. Aidha imani kamilifu iko ambayo ni ya wajibu au ukamilifu uliyopendekezwa.

Ni lazima maneno na matendo yaafikiane na Sunnah, vinginevyo hayazingatiwi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”[1]

Yule mwenye kuzungumza vizuri pasi na kunuia halipwi kitu. Yule mwenye kutenda matendo mema pasi na nia halipwi kitu. Yule mwenye kuswali, akafunga na akatoa swadaqah pasi na kunuia halipwi thawabu zozote. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vile alivyonuia.”

Isitoshe ni kwamba hayo yaliyotajwa ni lazima yaafikiane na Sunnah. Maneno na vitendo vinavyokwenda kinyume na Sunnah basi maneno na vitendo vyake ni batili na havina maana yoyote. Ndio maana baadhi ya wanachuoni wamesema:

“Imani ni kutamka kwa ulimi, kuamini ndani ya moyo na matendo ya viungo vya mwili pamoja na kuafikiana na Sunnah.”

Wazushi wanatoka nje ya maana hiyo. Wazushi hawana imani; ima hawana imani kabisa au wako na imani pungufu inayopungua kutokana na Bid´ah zao.

[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 73
  • Imechapishwa: 26/08/2021