Ni ipi hukumu ya kuvaa kanzu fupi na nguo ya mikono mifupi mbele ya Mahaarim?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa kanzu fupi na nguo ya mikono mifupi mbele ya Mahaarim?

Jibu: Mwanamke anatakiwa kusitiri mwili wake na wala asiwaonyeshe Mahaarim zake isipokuwa kile kitu kilichozoeleka kama vile uso, viganja vya mikono na miguu. Hivo ndio salama na kheri zaidi kwake.

Wanazuoni wametofautiana kuhusu yale anayotakiwa kuwaonyesha Mahaarim. Wanazuoni wengi wanaona kuwa inafaa kwake kuonyesha uso na viganja vya mikono. Wengine wakataja miguu. Wengine wakataja kichwa.

Kwa kumalizia ni kwamba anatakiwa kujihifadhi na atosheke kuonyesha uso, viganja vya mikono na miguu. Haja ikipelekea kuonyesha kitu katika kichwa hapana vibaya mbele ya Mahaarim; kama vile kaka yake na ami yake. Lakini bora zaidi hii leo ni mtu kuwa makini. Kuwa makini kwa baadhi ya Mahaarim ni bora zaidi. Kwa sababu baadhi ya Mahaarim hawana dini au dini yao ni chache. Kwa hivyo anatakiwa kuwa makini kutokana na jambo hili wakati wa kukaa naye chemba na awe katika upeo wa kujisitiri juu ya kitu ambacho pengine kikamtia katika mtihani. Uso na viganja vya mikono vinatosha na khaswa wale wasiokuwa na imani.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4310/ما-حكم-لبس-المراة-القصير-امام-المحارم
  • Imechapishwa: 16/06/2022