Ni bora kubeba jeneza juu ya mabega au juu ya gari?

Swali: Ni lipi bora kuibeba jeneza juu ya mabega au juu ya gari? Ni lipi bora kwenda kwa mbele au nyuma ya jeneza sawa iwe ni kwa kutembea au kupanda?

Jibu: Lililo bora ni kulibeba juu ya mabega kwa kuwa mtu anakuwa na mawasiliano na jeneza moja kwa moja. Sababu nyingine ni kuwa wale watakaoina jeneza watajua kuwa ni jeneza na watamuombea. Kadhalika ni jambo liko mbali na jeuri na kiburi. Hata hivyo ni sawa kulibeba jeneza juu ya gari ikiwa kuna haja au dharurah. Mfano wa hilo kama kuna mvua kali, joto kali, baridi kali au wabebaji wachache.

Kuhusu wakati wa kwenda, wanachuoni wametofautiana kama inatakiwa kuwa upande wake wa kulia, wa kushoto, nyuma yake au mbele yake. Watembeaji wanatakiwa kuwa mbele ya jeneza na walio juu ya kipando nyuma yake. Baadhi ya wanachuoni wanasema mtu aangalie lile ambalo ni sahali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/166)
  • Imechapishwa: 23/08/2021