Nguo inayovuka kongo mbili za miguu ni haramu katika hali zote

Swali: Je, kuvaa nguo inayovuka kongo mbili za miguu ni katika madhambi makubwa au maasi tu?

Jibu: Kunakhofiwa kuwa katika madhambi makubwa. Hilo ni kutokana na kemeo linalosema:

“Allaah hatomtazama siku ya Qiyaamah.”

Kufanya kiburi ni katika madhambi makubwa. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Imaam an-Nawawiy anaona kuwa inachukiza tu ikiwa mtu atavaa nguo inayovuka kongo mbili za miguu pasi na kivuli?

Jibu: Inahitaji kuangaliwa vyema. Maoni sahihi ni kwamba ni haramu kwa hali zote. Lakini mtu akivaa kwa kiburi jambo linakuwa khatari zaidi. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kilichoko chini ya kongo mbili za miguu katika kikoi ni Motoni.”

Hakufungamanisha na kiburi. Baadhi ya maandiko yanafasiri maandiko mengine. Maandiko yaliyoachiwa hayafasiri maandiko yaliyofungamanishwa katika hali hii. Yote haya ni matishio.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23302/ما-حكم-اسبال-الثياب
  • Imechapishwa: 22/12/2023