Swali: Ikiwa mtu anaweza kukemea maovu kwa moyo wake na hawezi kwa kutumia mkono wake na mdomo wake anaingia ndani ya yale waliyonyamazia maovu na adhabu inamkusanya au anakuwa miongoni mwa watakaookolewa na watengenezaji?

Jibu: Kuna ngazi mbalimbali za kukemea maovu, kama itakavyokuja huko mbele. Kuna wanaoweza kukemea kwa kutumia mkono au kwa mdomo. Vinginevyo angalau kwa uchache ni kwa moyo wake, hili hakuna asiyeliweza. Kukemea kwa moyo hakuna asiyeweza. Kuna ngazi  mbalimbali za kukemea maovu, kama itakavyokuja huko mbele – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (02)
  • Imechapishwa: 02/02/2024