Msimamo juu ya mzazi na ndugu wasioswali msikitini na kufanya maasi mengine

Swali: Baba na ndugu zangu hawaswali msikitini. Nimeshawanasihi mara nyingi lakini hawaitikii. Mara nyingi wakati ninaporudi kutoka msikitini namkuta baba yangu anavuta shisha na anatazama TV. Je, nikae nao baada ya hapo?

Jibu: Ni lazima kwako kuwanasihi na kuendelea kufanya hivo. Usiwaache.

Swali: Je, napata dhambi kwa kukaa nao?

Jibu: Kariri kuwanasihi na usinyamazie maovu. Usikatike moyo juu ya kuongoka kwao. Wafanyie subira. Kuhusu kukaa nao ikiwa unaweza kuhama na ukaeshi peke yako basi unalazimika kuhama. Usikae nao ilihali wako katika hali hii. Lakini ikiwa huwezi kukaa na kueshi peke yako, kaa nao na usubiri juu ya kuwanasihi na kuwakemea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (02)
  • Imechapishwa: 02/02/2024