Swali: Katika “Adab-ul-Mufrad” kumetajwa maneno yenye maana ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipita kati ya watu na baina yako alikuwepo mtenda dhambi mmoja ambapo akawapuuza na hakuwasalimia. Je, hapa kuna dalili ya kutomsalimia mtenda dhambi ikiwa anadhihirisha maasi?

Jibu: Ndio. Huku ni katika kuamrisha mema na kukataza maovu. Anayefanya maasi hadharani anakatwa. Katika kumsusa ni kutomtolea salamu ili arudi nyuma.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (02)
  • Imechapishwa: 02/02/2024