Swali: Je, hii leo kuna uwezekano kukawepo Malaika wanaopigana vita ikiwa kuna Jihaad inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah?

Jibu: Ambao wanapigana vita ni waumini. Kuhusu Malaika Allaah huwashusa ili kuwafanya imara na kuwatia nguvu waumini na kutia udhalilifu ndani ya mioyo ya makafiri. Vinginevyo wanaopigana vita ni waumini. Wao ndio wanaobeba silaha. Malaika wanawasapoti na kuwatia nguvu na kuweka woga ndani ya mioyo ya makafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (01)
  • Imechapishwa: 02/02/2024