Kulingana juu ya ´Arshi ni sifa ambayo Ahl-us-Sunnah wamejipambanua nayo. Watu wa Bid´ah wanapinga kwamba Allaah (Jalla wa ´Alaa) amelingana juu ya ´Arshi Yake. Kuna kundi katika wao ambao wamefasiri “kulingana juu ya ´Arshi” kwamba ni kutawala juu ya ´Arshi. Huku ni kumtukana Allaah (Jalla wa ´Alaa). Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“Hakika Mola wenu ni Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha akalingana juu ya ´Arshi.” (07:54)

Amebainisha kuwa kulingana juu ya ´Arshi ni jambo limetokea baada ya kutokuwepo kwake. Hivyo ikifasiriwa kwamba maana yake ni kutawala ni dalili yenye kuonesha kuwa kuna kipindi Allaah (Jalla wa ´Alaa) ambapo alikuwa hafanyi hivo. Huku ni kumtukana Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa sababu ni kumpokonya nguvu na umiliki Wake juu ya viumbe Wake wote. Hili linabainisha na kuthibitisha kwamba kulingana hakuna maana nyingine isiyokuwa ya ujuu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 73
  • Imechapishwa: 28/08/2020