Fawziy al-Bahrayniy amesema:

“Mdahalo na Rabiy´ al-Madkhaliy juu ya kuwatuhumu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwamba ni Baatwiniyyah, Raafidhwah…

Hili ni kosa kwa mitazamo miwili:

1- Maneno yake “… juu ya kuwatuhumu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwamba ni Baatwiniyyah, Raafidhwah… “

Allaah anajua kuwa nawaadhimisha, nawatukuza na kuwalinda Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah zaidi kuliko ninavyojilinda mwenyewe, watoto wangu na ndugu zangu. Naonelea kuwa mifumo yote inayoenda kinyume na ´Aqiydah yao ni mifumo ya upotevu na angamivu.

Nina – himdi zote ni za Allaah – vitabu vya kale na vipya ambapo nimebainisha na kutetea mfumo wa Salaf na kubainisha upotevu wa wapotevu na kukosoa misingi na mifumo yao. Nina mihadhara na darsa nyingi na zenye kuendelea juu ya hilo. Juhudi hizi zimeenea ulimwenguni kote.

Kwa ajili hiyo mapote yote, au basi angalau mengi, katika mapote ya kipotevu yananipiga vita kwa siri na kwa dhahiri katika vikao vyao, tovuti zao na darsa zao.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 10-11
  • Imechapishwa: 09/10/2016