12 – Wanashikamana na matamshi yenye kutia shaka ambayo yanaweza kuwa na maana nyingi. Wanadai kwa uongo ya kwamba Salaf walikuwa wanaonelea kuwa msemo “Jins-ul-´Amal”[1] unafanya nguzo katika katika kuiarifisha imani[2].

Uhakika wa mambo ni kuwa Salaf walikuwa wakitahadharisha matamshi yenye kutia shaka, kushikamana na matamshi yaliyowekwa katika Shari´ah yaliyothibiti katika Qur-aan na Sunnah na kumfanyia Tabdiy´ mwenye kutumia matamshi yenye kutia shaka. Tamko “Jins-ul-´Amal” halikutajwa si katika Qur-aan wala Sunnah. Maswahabah hawakulitumia wala Salaf hawakulitumia inapokuja katika masuala ya imani. Tamko hili ni lenye kutia mashaka. Kadhalika wameshikilia baadhi ya matamshi ya Ahl-us-Sunnah waliokuja nyuma ambayo hawana dalili yoyote kwayo, kwa sababu hawakuwa wakilenga yale ambayo Haddaadiyyah wanawatuhumu kwayo.

Nimeyabainisha haya kwa yule anayetaka haki. ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) alitahadharisha hilo na akabainisha ukhatari wake. Alisema kuwa utumiaji wa msemo huo na msemo “kitendo ni sharti ya kusihi kwa imani/kitendo ni sharti ya ukamilifu wa imani” malengo yake ni kumwaga damu na kuhalalisha mali. Lakini kama kawaida yao Haddaadiyyah wa sasa wakapuuzia mbali kufuata maneno ya wanachuoni ambayo hayaendani na matamanio yao. Hawakutosheka na hilo. Aidha wakaanza kumkashifu ´Allaamah Ibn ´Uthaymiyn kwa muda mrefu kwenye tovuti yao, kumtuhumu kuwa alitumbukia kwenye Bid´ah na kumraddi kwa aina ya kwamba:

“Mtu fulani na fulani anaafikiana na Shaykh Faalih na si Ibn ´Uthaymiyn.”

“Mtu fulani na fulani wanasema kuwa Ibn ´Uthaymiyn amekosea na kwamba Shaykh Faalih amepatia.”

Wanajaribu kumnyanyua mwongo na msaliti Faalih na kumwangusha Ibn ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah).

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/neno-jins-ul-amal-limetoka-kwa-murji-ah/

[2] Shaykh wao Faalih al-Harbiy alisema ibara hii ambapo Haddaadiyyah wakalisapoti, wakalieneza na kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah kwalo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 7-8
  • Imechapishwa: 09/10/2016