Fawziy al-Bahrayniy amesema:

“Mdahalo na Rabiy´ al-Madkhaliy juu ya kuwatuhumu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwamba ni Baatwiniyyah, Raafidhwah…

Hili ni kosa kwa mitazamo miwili:

2- Anawafanya Haddaadiyyah, ambao hawana kazi nyingine isipokuwa kuwapiga vita Ahl-us-Sunnah, kwamba ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Tangu walipozuka mpaka hii leo hiyo ndio sifa yao.

Ukiongezea kuwa ujinga na uongo wake umedhihiri pale anaposema kuwa mimi nawatuhumu Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah – Haddaadiyyah wenye chuki dhidi ya Ahl-us-Sunnah – kwamba ni Baatwiniyyah, Raafidhwah, Khawaarij, mayahudi na kadhalika. Huu ni uongo wa wazi. Niliandika makala nikionyesha kufanana kwa Haddaadiyyah na Raafidhwah. Sikusema kuwa wao ni Raafidhwah na Baatwiniyyah. Nililiweka wazi hilo kwenye makala hiyo hiyo. Mtu huyu kutokana na ujinga wa lugha ya kiarabu, ufahamishaji wa matamshi, istilahi za wanachuoni na kwamba ufananizi kati ya vitu viwili haupelekei kilichofananizwa kuwa hali kadhalika.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 11
  • Imechapishwa: 09/10/2016