Swali: Wakati baadhi ya watu wanapoambiwa kuwa ni wajibu kushikamana na dini kwa mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Salaf-us-Swaalih wanasema kuwa Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja katika “A´laam-ul-Muwaqqi´iyn” hali ambazo fatwa inabadilika zama hadi nyingine. Vipi kuraddi wanayosema?

Jibu: Fatwa sio mfumo. Mfumo unatakiwa kuwaw wa Salaf. 

Ama kuhusian na fatwa ambazo zinatokaman na Ijtihaad ambapo mwanachuoni anatoa fatwa kwa Ijtihaad na kisha anakuja kujua kitu ambacho alikuwa hakijui hapo kabla, halafu anatoa fatwa upya kwa kiasi na itakavyomdhihirikia. Hashikamani tu na ile fatwa ya kwanza. Pindi anapofikiwa khabari na kitu kipya anakitendea kazi. Hili halifuti ile fatwa ya kwanza; amesema alichoona katika wakati ule na hivi anasema anachoona sasa. Huu ni wajibu. Anashikamana na haki. Hakuacha haki. Sio haki ndio imebadilika. Ni Ijtihaad yake ndio imebadilika. Ijtihaad yake ndio imebadilika na sio zama. Mwanachuoni anaweza kujua kitu katika wakati ambapo asikijue katika wakati mwingine. Hatakiwi kushikamana kishabiki na maoni yake ya zamani. Anatakiwa kuhama na kutafuta haki. Akifikiwa na khabari ya kwamba fatwa hii ya mwisho ndio yenye nguvu kuliko ile ya kwanza, anatakiwa kushikamana nayo. Wanachuoni wanasema kuwa Ijtihaad haifuti Ijtihaad nyingine. Zote ni sahihi. Wakati ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alipotoa hukumu katika masuala fulani ambayo ilikuwa inatofautiana na hukumu yake ya hapo mwanzoni, akasema:

“Kile ni tulichohukumu hapo kabla na hichi tunahukumu sasa.”

Hakusema kuwa hukumu yake ya mwanzo ni batili, isipokuwa alisema tu kuwa hukumu ile ilitolewa kutokana na alivyokuwa anaonelea hapo kabla na hivi sasa ni kutokana na anavoonelea nyuma.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015