Swali: Baadhi ya watu wanafikiria kuwa mwanachuoni ni yule amehifadhi ikiwa ni pamoja na vile vitabu sita. Je, ni sahihi?

Jibu: Elimu sio kuhifadhi. Kuhifadhi ni njia tu, sio elimu kwa dhati yake. Elimu ni uelewa na ufahamu. Kuhifadhi ni njia tu inayopelekea katika elimu. Ni wangapi wenye kuhifadhi sana pasina ya kufahamu lolote! Wanahifadhi pasina kuelewa. Kwa sababu hawakutafuta uelewa, hamu yake kubwa ni kuhifadhi tu. Kuhifadhi hakutoshi. Sipuuzii kuhifadhi; ni vizuri. Lakini hata hivyo mtu asiridhike na hilo tu. Ni lazima aelewe Dini ya Allaah na afahamu aliyoyahifadhi. Mtu anatakiwa kukusanya kati ya kuhifadhi na kuelewa. Ni lazima iwe hivi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015