Ndani ya “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” kuna makosa

Swali: Ambaye yuko na kitabu “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” afaidike nacho au akichome moto?

Jibu: Sijakizingatia sana. Ndani yake kuna baadhi ya makosa. Kama ni mwanafunzi anaweza kukihifadhi na akafaidika nacho. Lakini kama sio katika wanazuoni atafute vitabu vya Salaf kukiwemo vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, vitabu vya Ibn-ul-Qayyim, vitabu vya Hadiyth na vitabu vya maimamu wanaotambulika. Kwa sababu ndani ya “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” kuna makosa. Mwanafunzi mwenye kufahamu anayatambua makosa. Ni vitabu vichache visivyokuwa na makosa isipokuwa Kitabu cha Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23425/حكم-اقتناء-كتاب-في-ظلال-القران
  • Imechapishwa: 17/01/2024