45. Hadiyth ”Waswalieni Manabii na Mitume wa Allaah… ”

45 – Muhammad bin Abiy Bakr al-Maqdamiy ametuhadithia: ´Umar bin Haaruun ametuhadithia, kutoka kwa Muusa bin ´Ubaydah, kutoka kwa Muhammad bin Thaabit, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

صلوا علي أنبياء الله ورسله فإن الله بعثهم كما بعثني

”Waswalieni Manabii na Mitume wa Allaah. Kwani hakika Allaah amewatuma kama alivyonituma mimi.”[1]

Allaah amsifu na amsalimishe yeye na wao.

[1] Cheni ya wapokezi wake ni nyonge sana. ´Umar bin Haaruun al-Balkhiy ni mwenye kuachwa na mwalimu wake Muusa bin ´Ubaydah ima ni kama yeye au ni mnyonge zaidi.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 48
  • Imechapishwa: 17/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy