44. Hadiyth ”Ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie… “

44 – Ibraahiym bin Hajjaaj ametuhadithia: Wuhayb ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من ذكرت عنده فلم يصل (عليَّ) فقد خطئ طريق الجنة

”Ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie, basi atapotea njia ya Peponi.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh, lakini kuna Swahabah aliyekosekana. Hapa kuna ufuatiliaji wenye nguvu kabisa wa Sulaymaan bin Bilaal, kutoka kwa Wuhayb bin Khaalid al-Baahiliy al-Miswriy. Hadiyth ni Swahiyh kama tulivyotaja kuhusu cheni ya kwanza ya wapokezi (41).

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 48
  • Imechapishwa: 17/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy