Je, maasi yote yanakuwa ni kufuru ndogo?

Swali: Je, maasi yote yanakuwa ni kufuru ndogo?

Jibu: Ni katika matendo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu… yanakuwa ni madhambi na maasi. Hayaitwi kuwa ni ´kufuru` isipokuwa yale ambayo Shari´ah imekuja kuyaita kuwa ni kufuru. Yale ambayo Shari´ah imeyaita kuwa ni ´kufuru` nawe utayaita. Kwa mfano:

“Mambo mawili kwa watu ni kufuru; kutukaniana nasabu na kuomboleza juu ya maiti.”

na:

“Msirejee baada yangu kuwa makafiri wapotevu baadhi wakizikata shingo za wengine.”

Kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah kutokana na matamanio na rushwa yote hayo yanaitwa kuwa ni kufuru.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23426/هل-جميع-المعاصي-من-الكفر-الاصغر
  • Imechapishwa: 17/01/2024