218 – ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

لتَنْهَكُنَّ الأصابعَ بالطّهورِ، أو لتَنْهَكنّها النارُ

“Hakikisheni mnasafisha vidole kwa maji, vinginevyo Moto utahakikisha unavichoma.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw” kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” ameipokea kutoka kwa Ibn Mas´uud[2] kwa cheni ya wapokezi nzuri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Katika upokezi mwingine kwenye “al-Mu´jam al-Kabiyr” Swahabah anasema:

خللوا الأصابعَ الخمسَ؛ لا يحشوها الله ناراً

“Sugueni kati ya vidole vitano ili Allaah asivichome Moto.”[3]

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Swahiyh.

[3] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/205-206)
  • Imechapishwa: 17/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy