Nasaha za Shaykh Rabiy´ kwa Salafiyyuun wa Tanzania


   Download

Himdi zote njema anastahiki Allaah. Swalah na salamu zimwendee Mtume wa Allaah, kizazi chake, Maswahabah zake na wale watakaofuata mwongozo wake.

Amma ba´d:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Enyi wapenzi! Namuomba Allaah anipe mimi na awape nyinyi tawfiyq na uthabiti katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah na kwa mfumo wa as-Salaf as-Swaalih na aturuzuku mimi na nyinyi elimu yenye manufaa na  matendo mema, atuwafikishe mimi na nyinyi kupendana kati yetu, udugu na kusaidiana katika wema na kumcha Allaah, atuepushe mimi na nyinyi shari ya fitina zenye kuonekana na zilizojificha.

Nawausia na kuiusia nafsi yangu kumcha Allaah (´Azza wa Jall), kuwa thabiti juu ya mfumo huu mtukufu, kufanya bidii katika kutafuta elimu kutoka katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaaah kwa mfumo wa as-Salaf as-Swaalih. Na kutoka vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyah na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahumaa Allaah). Nawasisitizia tena kufanya udugu mpaka muwe kama mwili mmoja na mujiepushe na sababu zote zinazopelekea katika za kutengana na fitina.

Namuomba Allaah atuthibitishe mimi na nyinyi katika haki na uongofu. Hakika Mola wetu ni Mwenye kuitikia du’aa.

Swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi  na Maswahabah zake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masjid Irshaad Ilala Dar es Salaam 1441 Rabiy´ ath-Thaaniy 07
  • Imechapishwa: 05/12/2019