Wanachuoni wamechukiza kufupiza kumswalia Mtume


Kilichowekwa katika Shari´ah ni kuandika kikamilifu kutokana na Allaah (Ta´ala) alivyoamrisha na msomaji akumbuke wakati wa kulipitia. Wala haitakikani wakati wa kuiandika kufupika kumswalia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa kuandika “SWA” au “S.A.W” na mfano wake katika ishara ambazo zinatumiwa na baadhi ya waandishi na watunzi wa vitabu. Hayo yanakwenda kinyume na amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Kitabu Chake kitukufu pale aliposema:

صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (33:56)

Pamoja na kwamba hakutimii malengo na kunakosekana fadhilah zinazopatikana katika kuandika “Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam” kikamilifu. Pengine hata msomaji asizinduke nalo au asifahamu makusudio yake licha ya kuwa wanachuoni wamechukizwa na kitendo hicho cha ishara na wakatahadharisha nacho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/old/33035
  • Imechapishwa: 05/12/2019