Nasaha za Ibn Baaz kwa anayetaka kumwacha mkewe mvivu

Swali: Nina mke anayetekeleza faradhi zote za dini, lakini hunilaumu katika baadhi ya mambo mpaka huzuka kinyongo. Hafanyi baadhi ya kazi isipokuwa kwa kinyongo, kwa kuwa amezoea uvivu. Je, inajuzu nimpe talaka?

Jibu: Unatakiwa uwe na subira ikiwa yeye ni mwema na mwenye dini – hata kama ana baadhi ya uvivu – inatakikana kwako uwe na subira. Wewe pia una baadhi ya uvivu. Hakuna yeyote aliyesalimika. Unapaswa uwe mwema na umsaidie katika kazi za nyumba. Msaidie. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwasaidia watu wa nyumbani kwake, naye ndiye bora wa viumbe. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwasaidia watu wa nyumbani katika mahitaji ya nyumba. Kwa hiyo wewe pia msaidie. Usiingize mtumishi. Msaidie ili asihitajie mtumishi. Msaidie katika mambo ya nyumba anayoshindwa nayo. Huenda akiwa na watoto ambao wamemchosha, msaidie katika kazi za nyumbani. Mtie moyo kwa maneno mazuri, sio kumtukana: ”Ee mwovu, ee mjinga” au maneno mengine. Bali mwambie: ”Ee binti fulani, mama fulani, simama tafadhali, Allaah akupa afya, Allaah akuridhie!” na maneno mengine mazuri.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1287/حكم-تطليق-الزوجة-بسبب-كسلها
  • Imechapishwa: 19/06/2026