Swali: Kuna mtu amesafiri kutoka Riyaadh kwenda Jeddah ili kushiriki mazishi ya mmoja wa jamaa zake. Alipowasili, watu wa nyumbani wakaamuru aswaliwe Haram na azikwe Makkah. Lakini huyu mtu hakuweka nia ya kufanya ´Umrah. Ni ipi hukumu?
Jibu: Ikiwa hakukusudia kufanya ´Umrah, basi hakuna tatizo. Kuingia Makkah si lazima kwa ajili ya ´Umrah au Hijjah. Ikiwa hakukusudia ´Umrah wala Hijjah, basi hakuna Ihraam juu yake. Ihraam ni kwa anayekuja Makkah kwa Hijjah au kwa kukusudia ´Umrah. Ama akija kwa ajili ya kushiriki jeneza, kwa biashara, kumtembelea jamaa au mambo mengine mfano wa hayo, basi hana wajibu wa kuingia katika Ihraam. Lakini lau angeweka nia ya kufanya ´Umrah, basi ingekuwa bora aingie katika Ihraam kutoka kwenye kituo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1311/حكم-دخول-مكة-لحاجة-غير-العمرة
- Imechapishwa: 19/06/2026
Swali: Kuna mtu amesafiri kutoka Riyaadh kwenda Jeddah ili kushiriki mazishi ya mmoja wa jamaa zake. Alipowasili, watu wa nyumbani wakaamuru aswaliwe Haram na azikwe Makkah. Lakini huyu mtu hakuweka nia ya kufanya ´Umrah. Ni ipi hukumu?
Jibu: Ikiwa hakukusudia kufanya ´Umrah, basi hakuna tatizo. Kuingia Makkah si lazima kwa ajili ya ´Umrah au Hijjah. Ikiwa hakukusudia ´Umrah wala Hijjah, basi hakuna Ihraam juu yake. Ihraam ni kwa anayekuja Makkah kwa Hijjah au kwa kukusudia ´Umrah. Ama akija kwa ajili ya kushiriki jeneza, kwa biashara, kumtembelea jamaa au mambo mengine mfano wa hayo, basi hana wajibu wa kuingia katika Ihraam. Lakini lau angeweka nia ya kufanya ´Umrah, basi ingekuwa bora aingie katika Ihraam kutoka kwenye kituo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1311/حكم-دخول-مكة-لحاجة-غير-العمرة
Imechapishwa: 19/06/2026
https://firqatunnajia.com/kuingia-makkah-kwa-haja-isiyo-umrah/