Nasaha kwa walinganizi na wanafunzi wanaokata ndevu

Swali: Tunaona baadhi ya walinganizi ambao wanawalingania watu wanaenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kufupisha ndevu. Je, inajuzu kwa walinganizi kufanya hivyo?

Jibu: Lililo la wajibu kwa walinganizi na wasiokuwa walinganizi ni kuzikirimu ndevu, kuziachia, kuzifuga na kutozifupisha. Hivi ndivyo alivoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema:

“Fupisheni masharubu na zirefusheni ndevu. Wakhalifuni washirikina.”

“Fupisheni masharubu na zirefusheni ndevu. Wakhalifuni majusi.”

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiamrisha kurefusha ndevu na kuzifuga na akikataza kuzifupisha, kuzikata na kadhalika. Kuzinyoa ndio kubaya zaidi na kukubwa zaidi. Kuzinyoa ni kubaya zaidi kuliko kuzifupisha. Japokuwa yote mawili ni haramu.

Wajibu kwa walinganizi ni mkubwa. Kwa kuwa wao ni walinganizi. Vilevile kwa mwanafunzi madhambi yanakuwa makubwa zaidi kuliko ambaye sio msomi. Japokuwa wote wawili ni wenye kupata madhambi katika aliyoharamisha Allaah. Lakini kufupisha ndevu kwa mwanafunzi madhambi yanakuwa makubwa zaidi. Kwa kuwa yeye ni kiigizo.

Swali: Shaykh! Wanasema kuwa Sunnah mtu haadhibiwi kwayo. Wanachukuliwa kuwa ni Sunnah.

Jibu: Mwenye kusema kuwa ni Sunnah hili ni kosa. Ni wajibu. Sunnah maana yake ni njia ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo anapata dhambi kwa yule mwenye kuiacha.

Isitoshe, lau tutakadiria kuwa ni jambo limependekezwa haikutakikana kwa walinganizi na wanafunzi kupuuza Sunnah ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha na akaita kwayo. Ni wajibu. Maamrisho yanaonesha uwajibu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 05/05/2015