Nasaha kwa anayependa sana mzaha

Swali: Mimi ni mtu ninayependa mzaha sana na wakati mwingine hutoka kwangu maneno yanayowaumiza baadhi ya ndugu bila kukusudia au hata kwa kukusudia. Unaninasihi nini?

Jibu: Tunakushauri kwanza upunguze mzaha. Jitahidi kupunguza mzaha; Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya mzaha, lakini kwa kiasi kidogo sana. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifanya mzaha, lakini hakuwa akisema isipokuwa haki tu. Hivyo jihadhari na kuzidisha mzaha, kwani huenda ukakupelekea kwenye shari. Unapofanya mzaha, basi jihadhari usiseme isipokuwa haki. Usimjeruhi ndugu yako wala usimuudhi kwa maneno yanayomdhuru au kusema kitu kisicho sahihi kumhusu.

Kwa ufupi mosi ni kwamba punguza mzaha, jambo ambalo ndilo linalotakiwa.

Pili ni kwamba unapofanya mzaha, basi sema haki tu na jihadhari kusema batili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3340/الاعتدال-في-المزاح
  • Imechapishwa: 14/08/2026