Shari´ah ya Allaah isimamishwe kwa wote

Swali: Je, kutekeleza mipaka ya Allaah katika nchi za kiarabu zinazotangaza kuwa dini ya dola ni Uislamu kunajuzu kutekelezwa kwa waislamu na wasiokuwa waislamu wanaoishi katika nchi hiyo?

Jibu: Ni wajibu kwa dola kutekeleza Shari´ah kwa waislamu na pia kwa wasiokuwa waislamu waliomo humo kama manaswara na mayahudi na kuchukua kodi kutoka kwao ikiwa wanaweza. Ikiwa hawawezi kuchukua kodi, basi wawape amani katika nchi na wawaache, ikiwa hawawezi kuchukua kodi. Lakini wanawazuia wasiwadhuru watu, wasiwadhulumu watu wala kuwaudhi watu. Kwa maana nyingine wanajitahidi kulinda usalama wa nchi dhidi ya maadui wa Allaah na wanawalazimisha waislamu kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayi wa sallam) na watekeleze juu yao adhabu kama kupigwa bakora mzinifu, kukatwa mwizi na mengineyo. Aidha wanawalazimisha watu kufuata amri za Allaah na kuwazuia na mambo aliyoyaharamisha Allaah. Makafiri waliopo wanawalazimisha kadiri ya uwezo wao kuzuia shari yao na madhara yao. Ikiwa wanaweza kuchukua kodi kutoka kwao kila mwaka – nayo ni mali inayowekwa juu yao kila mwaka – basi hilo ni wajibu. Ni wajibu kwa dola kuichukua kodi kutoka kwao kwa hali ya unyenyekevu wao mpaka wasilimu au watu wanufaike na mali hiyo pamoja na kuzuia shari yao.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3335/وجوب-تطبيق-الشريعة-على-المسلمين-وغيرهم-في-بلاد-المسلمين
  • Imechapishwa: 14/08/2026