Swali: Mimi ni kijana, kwetu kuna desturi kwamba kila usiku wa alkhamisi hukutana kwa mmoja wao, wanakesha wakicheza karata, kuvuta sigara, kuangalia video na kuzungumza maneno machafu. Je, inajuzu kukaa nao na kwenda katika vikao hivyo au nifanye nini?
Jibu: Hapana, hili halifai. Haya ni mambo ya maovu. Tayari umesikia mara nyingi kuwa haya hayafai. Linalotakiwa ni kuwaunga jamaa kwa njia ambayo haikufanyi ukubaliane na maovu wala kuhudhuria maovu. Unawanasihi na kuwaelekeza katika kheri na unawakataza vikao hivi ambavyo vina sigara, vilevi na vyombo vya upuuzi. Hivi ni vikao vya maovu, vikao vya shari na vikao vya kishaytwaan. Lakini wanasihi na waambie kwamba hayafai. Ni wajibu vikao vyenu viwe juu ya kheri na maneno mazuri, si juu ya yale aliyoyaharamisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Waelekeze wawe na vikao vya Qur-aan, Hadiyth nzuri na mazungumzo ya halali kuhusu mambo yao ya dunia na dini. Ama kukusanyika kwa ajili ya video za haramu, maovu, sigara, pombe au mfano wa hayo yaliyoharamishwa au kuwepo wanawake ambao hawakujisitiri, haya hayajuzu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3308/حكم-المكوث-في-مجالس-تقع-فيها-منكرات
- Imechapishwa: 14/08/2026
Swali: Mimi ni kijana, kwetu kuna desturi kwamba kila usiku wa alkhamisi hukutana kwa mmoja wao, wanakesha wakicheza karata, kuvuta sigara, kuangalia video na kuzungumza maneno machafu. Je, inajuzu kukaa nao na kwenda katika vikao hivyo au nifanye nini?
Jibu: Hapana, hili halifai. Haya ni mambo ya maovu. Tayari umesikia mara nyingi kuwa haya hayafai. Linalotakiwa ni kuwaunga jamaa kwa njia ambayo haikufanyi ukubaliane na maovu wala kuhudhuria maovu. Unawanasihi na kuwaelekeza katika kheri na unawakataza vikao hivi ambavyo vina sigara, vilevi na vyombo vya upuuzi. Hivi ni vikao vya maovu, vikao vya shari na vikao vya kishaytwaan. Lakini wanasihi na waambie kwamba hayafai. Ni wajibu vikao vyenu viwe juu ya kheri na maneno mazuri, si juu ya yale aliyoyaharamisha Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Waelekeze wawe na vikao vya Qur-aan, Hadiyth nzuri na mazungumzo ya halali kuhusu mambo yao ya dunia na dini. Ama kukusanyika kwa ajili ya video za haramu, maovu, sigara, pombe au mfano wa hayo yaliyoharamishwa au kuwepo wanawake ambao hawakujisitiri, haya hayajuzu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3308/حكم-المكوث-في-مجالس-تقع-فيها-منكرات
Imechapishwa: 14/08/2026
https://firqatunnajia.com/vikao-vya-ndugu-vya-kishaytwaan-unavyopaswa-kuepuka/