Swali: Katika mji wetu kuna Khawaarij wanaoeneza ufisadi. Mwishoni mwa mwaka huu, mwisho wa Ramadhaan, waliwaua watu waliokuwa wanaswali Tarawiyh. Je, inajuzu kuwaua watu hawa na ni ipi hukumu ya kushirikiana nao?

Jibu: Ndio, haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Wanawaua waumini na wanawaacha washirikina. Amesema kweli Mtume wa Allah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusiana na kuwaua, mamlaka, mtawala, ndiye anasimamia hilo. Watu hawapati kufanya hivo. Kwa sababu hili linapelekea katika machafuko. Mkiwaua na wao watakuueni na watawaua watoto wenu. Hili linapelekea katika machafuko na umwagikaji wa damu. Suala hili anarejelewa mtawala ikiwa kama kuna mtawala anayesimamisha adhabu [hadd]. Ikiwa hakuna mtawala, haijuzu kwa yeyote kusimamisha adhabu na kuua. Linapelekea katika machafuko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: at-Takfiyr bayn al-Ifraatw wat-Tafriytw