Ni wingi ulioje wa mijibwa ya Motoni ambao wanalipua katika miji ya Kiislamu baada ya kuajiriwa na watu wasiokuwa na urai katika nchi yoyote, wanafunzi wa mayahudi na manaswara, warithi wa wamasoni (freemasons) na mayahudi, wafanya kazi wa magharibi na mashariki. Wanatoa Fatwa kutoka kwenye milima ya makafiri na nchi za magharibini ambao wanawapa hifadhi na kuwatetea. Hasha juu yenu sehemu hizo ambazo wanaeneza sumu hii kwa Waislamu na wanawasaidia maadui wa Uislamu dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Allaah Amuue yule anayewafadhili! Allaah Amuue yule mwenye kuwanyamazia! Allaah Amuue yule anayeshirikiana nao! Allaah Amuue yule anayejiunga nao! Allaah Amuue yule anayewapa udhuru! Allaah Amuue yule anayewapa udhuru juu ya matendo yao! Allaah Amuue yule anayeona kuwa wako katika usawa! Allaah Amuue yule anayewakalia kimya tu!

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُ آثِمٌ قَلْبُهُ

“Na mwenye kuuficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi.” (02:283)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kunyamazia juu ya elimu, basi Allaah atamtolesha nayo kwa hatamu ya Moto siku ya Qiyaamah.”

Kwa sababu watu hawa ndio waovu kabisa wa viumbe. Ni nani aliyesema hivo? Ni nani ambaye aliwasifu kwamba ni viumbe waovu kabisa? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni nani aliyewasifu na kusema ni mijibwa ya Motoni? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni nani aliyewasifu kuwa wanatoka katika dini kama jinsi mshale unavotoka kwenye upinde wake na kwamba wanasoma Qur-aan na haivuki shingo zao? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni nani aliyewasifu ya kwamba wanawaua waislamu na wanawaacha washirikina? Ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni nani aliyesema wabaya kabisa ya wauliwaji ni wauliwaji wao, na kwamba wauliwaji wao ndio wabaya zaidi chini ya mbingu na kwamba mbora katika wauaji ni yule mwenye kuwaua? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ni wengi walioje leo – Allaah asiwafanye kuwa wengi. Bali wao ni wabaya zaidi kuliko hata Khawaarij wa zamani. Khawaarij wa zamani walikuwa na ´ibaadah, uchaji Allaah, kuipa nyongo dunia na uaminifu. Ama kuhusu hawa, ni waongo wakubwa na wanaonelea kuwa lengo linasahilisha njia.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=140126
  • Imechapishwa: 23/04/2015